Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 32 Water and Irrigation Wizara ya Maji 382 2026-05-19

Name

Fadhili Sandali Chilombe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE aliuliza: -

Je, lini Miradi ya Maji ya Tuwemacho, Masuguru-Mchoteka, Liwanga, Msinji na Azimio itakamilika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji napenda kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Fadhili Sandali Chilombe Mbunge wa Tunduru Kusini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Miradi ya Maji ya Tuwemacho, Masuguru-Mchoteka, Liwanga, Msinji pamoja na Azimio iliyopo katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma. Baadhi ya kazi zinazotekelezwa kupitia miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa vyanzo vya maji, ujenzi wa nyumba za mitambo kwa maana ya pump stations, ujenzi wa matenki matano ya kukusanyia maji (sump well) na kuhifadhi maji yenye jumla ya ujazo wa lita 1,250,000. Ulazaji wa mtandao wa mabomba umbali wa kilometa 59.9 sanjari na ujenzi wa vituo 20 vya kuchotea maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo miongoni mwake, Mradi wa Masuguru-Mchoteka umeanza kutoa huduma kwa wananchi wa vijiji vya Masuguru pamoja na Mchekeni wakati utekelezaji ukiwa ukiendelea. Serikali itatoa kipaumbele cha kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kadri zinavyopatikana ili iweze kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2026/2027 kama ilivyokusudiwa.