Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 32 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 384 2026-05-19

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kudhibiti watoa elimu ya afya na aina ya ulaji mitandaoni bila kuwa na taaluma inayotambulika jambo linalowachanganya wananchi?

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampenda kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua ongezeko la watu binafsi au wataalamu wanaotoa elimu au ushauri wa afya na lishe kupitia mitandao ya kijamii, hali inayoweza kupotosha na kuhatarisha afya za wananchi. Hii inatokana na kukua kwa uelewa wa masuala ya lishe, afya, utandawazi na ongezeko la vyombo vya kutolea habari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatekeleza Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009 Kifungu Namba 173(1) ambacho kinamtaka mtoa maudhui, mada au matangazo yanayohusu afya ya jamii kupata kibali kutoka kwa Waziri wa Afya au Afisa aliyeidhinishwa na Waziri. Kushindwa au kwenda kinyume na sheria hii mtoa maudhui au mtoa mada atachukuliwa hatua za kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha. (Makofi)