Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 14 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 162 | 2026-04-22 |
Name
Mattar Ali Salum
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shaurimoyo
Primary Question
MHE. MATTAR ALI SALUM aliuliza:-
Je, Serikali haioni haja ya kufanya ZEMA kuwa Wakala wa NEMC ili kuratibu na kusimamia kwa ufanisi Miradi inayotekelezwa upande wa Zanzibar?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais, Muungano na Mazingira, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mattar Ali Salum, Mbunge kutoka Shaurimoyo Zanzibar kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Sura 191 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Zanzibar ya mwaka 2015 zimeanzisha taasisi mbili za usimamizi wa masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini. Taasisi hizo ni Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa upande wa Tanzania Bara na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) kwa upande wa Zanzibar.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taasisi hizi zimekuwa zikishirikiana kwa ufanisi katika kusimamia mazingira hususan katika masuala yafuatayo: kwanza, zimekuwa zikishirikiana kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo; pili, zimekuwa zikitafuta fedha za uhifadhi na usimamizi wa mazingira kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo; pamoja na kubadilishana utaalamu na uzoefu kuhusu masuala ya usimamizi wa Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika kuimarisha ushirikiano pamoja na hatua hizo zilizochukuliwa, taasisi hizi mbili zipo katika taratibu za kuanzisha makubaliano rasmi ya ushirikiano ambayo yanalenga kuimarisha usimamizi wa mazingira katika pande zote mbili za Muungano na nchi zetu kwa ujumla. Hivyo, kutokana na ushirikiano huo, Serikali za pande zote mbili hazioni haja ya kuifanya ZEMA kuwa Wakala wa NEMC.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved