Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mattar Ali Salum
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shaurimoyo
Primary Question
MHE. MATTAR ALI SALUM aliuliza:- Je, Serikali haioni haja ya kufanya ZEMA kuwa Wakala wa NEMC ili kuratibu na kusimamia kwa ufanisi Miradi inayotekelezwa upande wa Zanzibar?
Supplementary Question 1
MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini nina maswali kwa Mheshimiwa Waziri. Ninaomba kufahamu commitment ya Serikali, lini makubaliano haya yatakuwa yamekamilika?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili pia, ninaomba commitment ya Serikali kwamba hii NEMC lini itakuwa Mamlaka kamili?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijayajibu maswali ya Mheshimiwa Mattar nimshukuru sana na kumpongeza kwani amekuwa ni sehemu ya Wabunge kutoka Zanzibar, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambavyo Wabunge wote wanaowakilisha Zanzibar kwenye Bunge hili, wamekuwa ni watu watetezi wazuri wa upande wa pili wa Muungano. Ametaka kujua ni lini makubaliano kati ya ZEMA na NEMC yatatekelezwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali zote mbili na Mamlaka hizi mbili zimeshaandaa MOU (Memorandum of Understanding) ya namna gani wataweza kutekeleza majukumu kwa pamoja katika uhifadhi wa mazingira ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya kushirikiana ZEMA kutoka Zanzibar na NEMC kutoka huku kwetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, makubaliano haya yameshakamilika. Hivi sasa pande zote mbili zinayapitia ili kama kuna jambo la kuongeza ama la kupunguza waweze kukubaliana na baada ya hapo tutakwenda kwenye kusaini makubaliano hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili la nyongeza ametaka kujua, ni lini NEMC itakuwa mamlaka kamili? Mheshimiwa Waziri wetu wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Eng. Masauni jana amesimama hapa, amesoma bajeti yetu ya Wizara na katika mambo ambayo yamesomwa kwenye bajeti ile ni jambo hili la NEMC kuwa Mamlaka kamili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Hotuba ile tumeahidi hapa Bunge lijalo ambalo ni Bunge la Miswada ya Serikali, italetwa hapa Muswada ili Bunge hili liridhie NEMC kuwa Mamlaka kamili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved