Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 14 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 163 2026-04-22

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Missenyi utakamilika ikizingatiwa kuwa ujenzi huo umechukua muda mrefu sana?

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu swali namba 163 la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Jimbo la Missenyi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Missenyi ni sehemu ya mpango wa Serikali wa ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) 65 katika Wilaya 64 na Mkoa mmoja wa Songwe. Utekelezaji wa mpango huu unafanyika katika Wilaya na Mkoa ambao bado hauna Vyuo hivi. Lengo ni kuhakikisha fursa za mafunzo ya ufundi stadi zinasogezwa karibu na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Missenyi ambacho kinatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2026. Hadi sasa, Serikali imeshatumia jumla ya shilingi bilioni 1.0 kati ya shilingi bilioni 1.6 zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huu. Ujenzi umefikia 65% ya utekelezaji wake.