Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Florent Laurent Kyombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Missenyi utakamilika ikizingatiwa kuwa ujenzi huo umechukua muda mrefu sana?
Supplementary Question 1
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Missenyi nishukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifanya Missenyi ikawa miongoni mwa Wilaya 64 ambazo zinapata Miradi ya Chuo cha VETA. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niupongeze Uongozi wa Wizara ya Elimu chini ya Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda na pia Naibu Waziri. Chuo hiki cha VETA kwa muda mrefu kilidorora katika ujenzi, lakini nikupongeze Mheshimiwa Naibu Waziri, baada ya kwenda ofisini kwake na kueleza, aliwapigia simu wasaidizi wake; na nimhakikishie, hata vifaa wiki iliyopita semi-trailer imeshusha vifaa, ujenzi unaendelea kama alivyosema. Kwa hiyo, Wanamissenyi wana matarajio kwamba hii 65% na 60% ambayo unaisema, Chuo kitakamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu mawili ya nyongeza. Kwa kuwa tunaona kwamba Chuo kinaenda kukamilika mwezi wa Saba, je, hatuwezi kuanza kufanya usaili wa wanafunzi ili chuo hicho kikikamilika wanafunzi waanze moja kwa moja?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa kukamilika ujenzi bado tunahitaji vifaa na walimu, je, Serikali inatoa commitment gani kuhakikisha kwamba Chuo hicho kitaanza kutumika lini? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Wanu Hafidh Ameir
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimjibu maswali ya nyongeza Mheshimiwa Florent Kyombo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kama nilivyojibu katika swali langu la msingi kwamba chuo hiki kinatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba, 2026 kwa awamu ya kwanza kwa kukamilisha majengo ya Utawala, Vyoo, Karakana, Mifumo ya Umeme na Maji, baada tu ya kukamilika Chuo hiki, basi kitaanza kutoa mafunzo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kwamba kwa kawaida mafunzo ya VETA huanza kila mwezi Januari wa kila mwaka. Kwa hiyo, kwa kuwa Chuo kinamalizika Septemba, 2026 tunategemea kwamba mpaka Januari, 2027 Chuo kitaanza kutoa mafunzo haya. (Makofi)
Name
Ado Shaibu Ado
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Missenyi utakamilika ikizingatiwa kuwa ujenzi huo umechukua muda mrefu sana?
Supplementary Question 2
MHE. ADO S. ADO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Wilaya ya Tunduru ni moja kati ya Wilaya ambazo hazina Vyuo vya VETA, na kwa kuwa ujenzi wa awamu ya kwanza wa Chuo cha VETA, Tunduru unaohusisha majengo tisa mpaka sasa bado unasuasua, kwani ulipaswa kukamilika mwaka 2024 lakini mpaka sasa haujakamilika, ni ipi kauli ya Serikali juu ya kukamilishwa kwa Chuo cha VETA Tunduru?
Name
Wanu Hafidh Ameir
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika jibu langu kwenye swali la msingi, tunatarajia vyuo hivi kukamilika Septemba, 2026. Hata hivyo, ahadi ya Serikali ni kwamba baada ya Bunge hili nitafanya ziara mahususi ya kupitia Vyuo hivi na kuona maendeleo ya vyuo hivi ili tuone wapi tunakwamua, pale vyuo hivi vilipokwama. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved