Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 14 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 167 | 2026-04-22 |
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vihenge vya Kisasa (maghala) vya kutunzia mazao vilivyopo eneo la TAZARA Isangi Mbozi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Ujenzi wa Vihenge vya Kisasa (maghala) vya kutunzia mazao vilivyopo eneo la TAZARA Isangi Mbozi ni mojawapo ya miradi ya ujenzi wa vihenge na maghala ya kisasa unaotekelezwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa vihenge hivyo ulikuwa ukitekelezwa na Kampuni ya Feerum S. A. ambayo ilishindwa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na hatimaye Serikali ilisitisha mkataba wake ukiwa umefikia 74% ya utekelezaji mnamo Oktoba, 2024. Baada ya hatua hiyo, mkandarasi mpya Unia Araj amepatikana na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo ifikapo Juni, 2027.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved