Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vihenge vya Kisasa (maghala) vya kutunzia mazao vilivyopo eneo la TAZARA Isangi Mbozi?
Supplementary Question 1
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri na yenye matumaini. Ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa kuwa sasa mkataba mpya wa Kampuni hii ya Unia Araj umeshasainiwa, je, una thamani ya shilingi ngapi ili mradi huo uweze kukamilika? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa ujenzi huu umechukua muda mrefu sana na ulikuwa unatekelezwa kama ulivyosema na Kampuni ya Feerum, ambayo toka mwaka wa 2021 ilitangaza kwamba imefilisika na ikaacha kutekeleza miradi yote mitano katika maeneo ya mikoa mbalimbali, na sababu zilizotolewa ilikuwa ni kwamba anadai fedha zilizobaki hazitoshi kukamilisha mradi huo, sasa swali langu, je, Serikali imeshapata fedha za ziada kutoka wapi ili ziweze kutumika kukamilisha mradi huo? Ahsante. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Mbozi kwa maswali ya msingi, na kiukweli amekuwa akipigania jambo hili Mbunge wa Vwawa Mheshimiwa Hasunga kuhakikisha kwamba Mradi huu wa Vihenge unakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja tu ambalo ninataka nimhakikishie, moja, thamani ya mradi ambao sasa kwa sababu ni vihenge vyote ambavyo vilikuwa chini ya Feerum, tumesaini mkataba mpya wa dola milioni 38, ambao sasa utakamilisha vikiwemo hivi vya Mbozi na maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu fedha, tunayo, kwa sababu NFRA wamekuwa wakifanya biashara ya mahindi na wewe unafahamu, na ndiyo maana wamenithibitishia. Nimeongea na Mkurugenzi mimi mwenyewe akaniambia vitakamilika kama ambavyo tumesaini katika huu mkataba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa sasa hivi fedha ipo na mradi ule utakamilika kama ambavyo sisi Serikali tumepanga. Kwa hiyo, niwathibitishie tu wananchi wa Vwawa na Mkoa wa Songwe kwamba, Vihenge vile vitakamilika kwa wakati na watafanya biashara yao kwa uhakika. (Makofi)
Name
Johannes Lembulung’ Lukumay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vihenge vya Kisasa (maghala) vya kutunzia mazao vilivyopo eneo la TAZARA Isangi Mbozi?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. JOHANNES L. LUKUMAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Jimbo la Arumeru Magharibi lina wakulima wazuri sana wa mbogamboga, lakini hili jimbo lina miundombinu ambayo hairidhishi hasa ya umwagiliaji, hususan uboreshaji wa mifereji ya asili. Je, ni lini Serikali itajenga Skimu Majimoto?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mbunge wa Arumeru Magharibi kwamba, mpango wa Serikali ni kuhakikisha tunajenga miradi ya umwagiliaji maeneo yote nchini ili kuhakikisha kwamba tunaongeza tija kwa mkulima, na mkulima analima katika kipindi chote cha mwaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika eneo lako la Arumeru, na moja ya maelekezo ambayo tulipewa sasa hivi ni kuhakikisha moja, tunakwenda kwenye ile tunasema miradi ya asili. Kuna ile umwagiliaji ama Schemes za asili, tuhakikishe tunaziboresha kwa gharama nafuu ili zianze kuleta matokeo makubwa haraka, wakati huo huo tukiendelea na hii miradi mikubwa ambayo inafanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Wanaarumeru Magharibi wako sehemu ya mpango wa Serikali kutekeleza hilo. Kwa hiyo, ninamthibitishia tu kwamba tuko kwenye kazi.
Name
Esther Nicholas Matiko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tarime Mjini
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vihenge vya Kisasa (maghala) vya kutunzia mazao vilivyopo eneo la TAZARA Isangi Mbozi?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Soko la Kimataifa la Mazao la Lemagwe ni muhimu sana kwa uchumi wa Tarime, Mara, na Taifa, na ujenzi ule wa Soko la Kimataifa unaenda sambamba na ujenzi wa ghala. Ninataka kujua, ni lini sasa unaenda kukamilika baada ya kuwa umesimama kwa muda na mmesainisha mwaka 2025 mkataba? Lini wananchi wa Tarime wanategemea Soko la Kimataifa linaenda kukamilika sambamba na ghala? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, niwathibitishie tu wananchi wa Tarime kwamba, Soko la Lemagwe tulishasaini mkataba, ambacho kilikuwa kimechelewa ilikuwa ni fedha na tayari tulishaomba fedha Wizara ya Fedha na wametuthibitishia kutupatia kwa ajili ya kumkabidhi mkandarasi na kuanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunatarajia kwamba mradi ule utakamilika kwa wakati, na kama utachelewa, basi kutakuwa na extension ya muda usiozidi miezi sita kabla ya ule mradi kukamilika.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved