Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 14 Water and Irrigation Wizara ya Maji 168 2026-04-22

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya shilingi bilioni 4.5 kwa wananchi wa Mji wa Karatu ili waweze kupata huduma ya uhakika ya majisafi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Awack, Mbunge wa Jimbo la Karatu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayolenga kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wa Karatu Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025 hadi sasa, jumla ya shilingi bilioni 1.742 zimetolewa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA) ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya kuboresha huduma ya maji katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hizo zimewezesha kukamilisha utekelezaji wa miradi ya maji Ayalabe, Bwawani Namba tatu sambamba na uchimbaji wa visima vitatu vya Endoro, Maliasili pamoja na Tom III ambapo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha maji lita 200,000 kwa saa. Vilevile, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya maji Karatu Mjini wenye thamani ya shilingi 864,822,827.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi ya maji katika Jimbo la Karatu kadiri fedha zinavyopatikana ili kuhakikisha miradi inayoendelea inakamilika.