Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 509 2026-06-04

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Vwawa – Londoni – Msia hadi Isalalo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa Barabara ya Vwawa – Londoni mpaka Msia yenye urefu kilometa 13.7 ambayo inahudumiwa na TARURA na kutoka Msia hadi Isalalo yenye urefu wa kilometa 20.5 inahudumiwa na TANROADS. Kutokana na umuhimu wa Barabara ya Vwawa – Londoni hadi Msia, imeingizwa kwenye Mradi wa TACTIC unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Kwa awamu ya kwanza barabara hiyo itajengwa kwa urefu wa kilometa 2.0 kwa kiwango cha lami kuanzia Vwawa.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara ya Vwawa – Londoni mpaka Msia yenye urefu wa kilometa 13.7 iliyopo katika Wilaya ya Mbozi, Serikali imeendelea kuihudumia, ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali ilitenga jumla ya shilingi milioni 17.65 kupitia Mfuko wa Barabara (Road Fund) kwa ajili ya kuchonga barabara hiyo kwa urefu wa kilometa 6.0 na kuzibua makalvati pamoja na mifereji ya maji ya mvua.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 36.69 kupitia fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund) kwa ajili ya kuchonga barabara kwa urefu wa kilometa 6.14, na kujenga box culvert mistari miwili.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuzihudumia barabara katika Jimbo la Vwawa ikiwemo Barabara ya Vwawa-Londoni-Msia ili ziweze kupitika muda wote.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.