Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Vwawa – Londoni – Msia hadi Isalalo?

Supplementary Question 1

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwanza naishukuru Serikali kwa majibu mazuri ambayo yametolewa.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa katika maeneo ambayo Serikali tayari imetenga shilingi milioni 17.6 kwa ajili ya ujenzi wa mifereji pamoja na makalvati yalijengwa chini ya kiwango, mifereji iko juu barabara iko chini, kwa hiyo, maji yanarudi kwenye barabara badala ya kutoka nje. Je, Serikali iko tayari sasa kuongeza usimamizi ili mifereji hiyo ijengwe kwa kiwango kinachotakiwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tunashukuru kwa mpango wa kutujengea kwamba mtajenga kilometa mbili kwenye Mradi ule wa TACTIC kilometa mbili, lakini kilometa mbili hazitufikishi kwenye eneo ambalo ni baya sana la Mto Nkana ambalo liko karibu kilometa nne, je, Serikali iko tayari kuongeza kilometa badala ya kuwa mbili ziwe tano ili tufike eneo ambalo ni baya sana wakati wa masika ili liweze kupitika?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Hasunga, Mbunge wa Jimbo la Vwawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nakubaliana naye kwamba maeneo ambayo kuna usimamizi ambao si thabiti unaleta changamoto ya ukamilishaji wa miradi hii. Kupitia Bunge lako Tukufu na kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, nimuelekeze Meneja wa TARURA Mkoa afike eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge ameliainisha ili kuweza kufanya tathmini na kuona uhalisia wa jambo ambalo Mheshimiwa Mbunge ameliwasilisha hapa na Serikali tuweze kuchukua hatua.

Mheshimiwa Spika, swali la pili nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa kuwa barabara hii sasa tumeihamishia TACTIC, fedha hizi za uhakika zinazotoka World Bank, tuendelee kuwa na subira kwa ujenzi wa kuanza na hizi kilometa mbili na tutaendelea kutenga fedha kuhakikisha Mheshimiwa Mbunge tunakamilisha adhma ya kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami na ili iweze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi wa jimbo la Vwawa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Vwawa – Londoni – Msia hadi Isalalo?

Supplementary Question 2

MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Kakonko tunashukuru sana Serikali kwa kutujengea kilometa tatu za lami kuelekea hospitali ya wilaya, ukiacha barabara hiyo mtandao wa lami katika Mji wa Kakonko ambao ndiyo makao makuu ya wilaya tuna meta 950 peke yake. Kwa kuwa moja ya ahadi ya kiongozi wa nchi ilikuwa ni kuongeza mtandao wa barabara za lami, ni upi mpango wa Serikali kuhakikisha sasa Makao Makuu ya Wilaya ya Kakonko yanaongezewa barabara kwa kiwango cha lami?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Alan, Mbunge wa Jimbo la Kakonko na nimpongeze kwa kuendelea kuwapambania wanajimbo la Kakonko na wanajimbo wanafahamu Mbunge wao kwa namna gani anavyowasilisha changamoto za jimbo na sisi kama Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kutenga bajeti na kuhakikisha tunafanya ujenzi katika barabara hizo ambazo Mheshimiwa Mbunge umeziainisha.

Mheshimiwa Spika, ni mpango wa Serikali kila halmashauri na makao makuu ya halmashauri kuendelea kujenga barabara hizi kwa kiwango cha lami angalau kwa awamu kwa kila mwaka ili kuhakikisha halmashauri zetu zinapata huduma hii na zinakuwa smart. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali itaendelea kumpa ushirikiano kuhakikisha kwamba tunajenga barabara hizo na zinatoa huduma iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Vwawa – Londoni – Msia hadi Isalalo?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, barabara ya kutoka Kata ya Mletele kwenda Kata ya Mshangano ndio mkombozi katika Manispaa ya Songea kipindi cha masika wakati barabara kubwa inajifunga.

Je, ni lini sasa Serikali itajenga barabara hii ya kutoka Kata ya Mletele kwenda Kata Mshangano kwa kiwango cha lami?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha tunajenga barabara hizi kwa kiwango cha lami, barabara ambayo ameiainisha; kwanza tunaanza na moramu, changarawe ili kuweza kuziweka katika huduma bora na ziendelee kutoa huduma kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kumpa ushirikiano kuhakikisha kwamba tunazijenga barabara hizi ili ziweze kupitika masika na kiangazi na zitoe huduma ambayo Serikali imekusudia.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Name

Kija Limbu Ntemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katoro

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Vwawa – Londoni – Msia hadi Isalalo?

Supplementary Question 4

MHE. KIJA L. NTEMI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Waziri katika Mji wa Katoro barabara nyingi bado zina changamoto ya kupitika. Je, ni lini sasa Serikali itaingiza Mji wa Katoro katika mfumo wa TACTIC ili uweze kujengwa na kutengenezwa kwa haraka ili kuwapunguzia wananchi wa Katoro adha ya barabara mbovu ambazo zipo katika Mji wa Katoro?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kija Limbu Ntemi, Mbunge wa Jimbo la Katoro na nimpongeze kwa namna ambavyo anaendelea kufuatilia changamoto za Jimbo la Katoro.

Mheshimiwa Spika, Katoro ipo chini ya Mamlaka ya Mji Mdogo na huwa inaendelea kupokea zile barabara ambazo ni za kuendeleza Mamlaka ya Miji Midogo, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kutenga bajeti kuhakikisha kwamba, mji wetu wa Katoro na ongezeko kubwa la watu na aina ya jiografia kwa sababu ya mmomonyoko wa ardhi, kwa sababu ya mvua zinazoendelea kunyesha, tutaendelea kuufanya mji wetu uwe bora na uweze kupitika nyakati zote za masika na kiangazi, ili sasa ile huduma ambayo imekusudiwa ya kutoa huduma bora za barabara Jimbo la Katoro liweze kupitika maeneo yote.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kija Limbu Ntemi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI tutaendelea kumpa ushirikiano na kujenga barabara hizo. Naomba kuwasilisha.