Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 510 2026-06-04

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:-

Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, Mbunge wa Jimbo la Karatu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikijenga shule mpya za sekondari, kuongeza miundombinu katika shule zilizopo ili kuendana na ongezeko la wanafunzi.

Mheshimiwa Spika, kati ya mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026 Serikali imepeleka jumla ya shilingi bilioni 1.63 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya tatu za sekondari, madarasa 116, maabara 17, matundu ya vyoo 182, mabweni 11 na nyumba za walimu 10 zilipokea jumla ya shilingi milioni 79.

Mheshimiwa Spika, narudia, kati ya mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026 Serikali imepeleka jumla ya shilingi bilioni 1.63 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya tatu za sekondari, madarasa 116, maabara 17, matundu ya vyoo 182, mabweni 11 na nyumba za walimu 10 katika Shule za Sekondari za Halmashauri ya Karatu. Shule za Matala na Lositete zilipokea jumla ya shilingi 79,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa moja na matundu ya vyoo mawili katika Shule ya Matala na ukamilishaji wa nyumba moja ya mwalimu na chumba kimoja cha darasa katika Shule ya Lositete.

Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 452.6 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 30, maabara nne, darasa moja, nyumba moja ya mwalimu na vitanda 120 katika Shule za Sekondari ya Wilaya ya Halmashauri ya Karatu. Shule za Matala na Lositete zitapokea jumla ya shilingi 145,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa maabara moja katika Shule ya Matala na maabara moja na darasa moja katika Shule ya Lositete.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya na kuongeza miundombinu katika shule zilizopo ili kuendana na ongezeko la wanafunzi. Naomba kuwasilisha.