Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Moshi Selemani Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanganyika
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?
Supplementary Question 1
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa juhudi zilizofanywa na Serikali zimeonekana na tunashukuru kwa kazi kubwa ambayo imefanyika, lakini bado kuna uhitaji mkubwa wa tatizo la vyumba vya madarasa, sambamba na ukosefu wa nyumba za walimu. Nini tamko la Serikali kumaliza tatizo hilo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ina shule ambazo zina tatizo kubwa na upungufu mkubwa wa madawati na vyumba vya madarasa kwenye Kata ya Kapalamsenga na Kata ya Kamsanga. Ni lini Serikali itapeleka fedha hizo kwa ajili ya kutatua kero ya uhaba wa vyumba vya madarasa? (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali madogo ya nyongeza yaliyoulizwa na Mheshimiwa Mbunge Kakoso kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutenga fedha na imeendelea kuainisha mipango thabiti kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pamoja na nyumba za watumishi. Katika Bunge lako Tukufu nilikwishaeleza mpango mahsusi ambao tulienda nao pale Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kuhakikisha kwamba sasa tunaenda kuanza kwa awamu ujenzi wa nyumba za watumishi 2,000 ambazo tutashirikisha sekta binafsi ili kuhakikisha kwamba nyumba hizi tunazikamilisha kwa wakati na watumishi wetu wapate nyumba hizi, ili waweze kufundisha watoto wetu kwa utulivu.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya madawati na kujenga madarasa, na mpango uliopo, madarasa ya sasa yakijengwa lazima yawe na madawati angalau 45 ili kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaanza kupata huduma.
Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali itaendelea kufanya juhudi hizi ili kuona kwamba tunajenga madarasa ambayo yanakuwa na madawati ili watoto wetu wapate mahali salama pa kujifunzia. Naomba kuwasilisha.
Name
Bakari Bakari Shingo
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Ukonga
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?
Supplementary Question 2
MHE. BAKARI B. SHINGO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitoe shukrani sana kwa ufafanuzi kutoka TAMISEMI juu ya kero ya michango shuleni na nina uhakika sasa, tunaenda kumaliza karaha ya michango isiyokuwa na maana ambayo mingi imekuwa inaleta lawama kwa Serikali yetu.
Mheshimiwa Spika, nilitaka nifahamu mpango wa Serikali baada ya mvua kuharibu barabara zetu huko mitaani, hasa katika Jimbo langu la Ukonga. Ni lini sasa Serikali wataanza kusambaza kifusi kwa ajili ya kujaza hizo barabara hasa za kule Ulongoni A, Ulongoni B, Barabara ya Mwembe Supu kuelekea kule Mwembe Samaki. Naomba Mheshimiwa Waziri atueleze kwamba karaha hii inakuwaje ili tuweze kuondokana na mashimo ambayo…
SPIKA: Mheshimiwa Shingo swali lako umeuliza la barabara siyo?
MHE. BAKARI B. SHINGO: Mheshimiwa Spika, naam.
SPIKA: Swali lako ni kifusi cha barabara?
MHE. BAKARI B. SHINGO: Mheshimiwa Spika, kifusi kwenye barabara zetu ambazo ziko chini…
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shingo kama ifuatavyo:-
Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekiri, Serikali tumetoa maelekezo mahususi kuhusiana na michango holela shuleni; lakini suala lake la barabara, kwanza nimwelekeza Meneja wa TARURA Wilaya, afike eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge ameainisha na achukue hatua za dharura kuweza kusambaza vifusi hivi, ili wananchi waendelee kupata huduma stahiki. Naomba kuwasilisha.
Name
Tinnar Andrew Chenge
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?
Supplementary Question 3
MHE. TINNAR A. CHENGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Simiyu ina wanafunzi ambao wana ulemavu, je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya miundombinu wezeshi ili wanafunzi hawa, waweze kwenda darasani na hasa katika kipindi cha mvua?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Tinnar Chenge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza miundombinu ya shule na miundombinu inayotoa huduma katika jamii zetu, yote imejengwa ili iweze ku-accommodate walemavu katika jamii zetu. Kwa hiyo, nimwelekeze mkurugenzi, afike katika shule ambayo Mheshimiwa Mbunge ameiainisha, ili kwanza kujiridhisha kama kweli miundombinu haipo; na kama haipo achukue hatua za dharura kuweza kuweka miundombinu hii, ili vijana wetu walemavu wanaopata elimu katika shule hizi waweze kupata elimu bila changamoto yoyote. Naomba kuwasilisha. (Makofi)
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?
Supplementary Question 4
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona. Shule ya msingi iliyoko katika Kata ya Mtakilwa, Jimbo la Tabora Mjini, ina upungufu mkubwa sana wa madarasa. Kuna madarasa matano peke yake, hivyo kupelekea wanafunzi kusoma kwa awamu. Ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba wanaongeza madarasa ili wanafunzi waweze kusoma kila mwanafunzi na darasa ambalo anatakiwa awepo?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI tayari imeshaandaa mpango wa kuhakikisha kwamba shule hii tunakwenda kuiongezea madarasa, ili wanafaunzi wetu waweze kusoma bila changamoto yoyote. Naomba kuwasilisha. (Makofi)
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?
Supplementary Question 5
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Jimbo la Morogoro Kusini lina kata 17 na takribani katika kila kata tayari wananchi wameshajenga maboma ya madarasa na sasa wanasubiri pesa za kumalizia kutoka Serikalini.
Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini sasa mtatuingizia pesa ili tuweze kumaliza vyumba hivyo vya madarasa?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mfaume, Mbunge wa Jimbo la Morogoro.
Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi kwa kuweka nguvu zao na kwenda kujenga maboma hayo na ni maelekezo mahususi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kwamba kabla ya kuanza miradi mipya, tuhakikishe maboma yote tunayakamilisha na yanatoa huduma tarajiwa.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa jimbo, tunakwenda kukamilisha maboma haya ili kuhakikisha kwamba yanaanza kutoa huduma kwa wakati na tukielekea mwaka 2028 ambapo tutapokea double cohort ya wanafunzi darasa la sita na la saba wote watamaliza kwa pamoja, kwa hiyo, ni lazima tuhakikishe miundombinu hii tunaikamilisha kwa wakati ili ikatoe huduma kwa wananchi wetu. Naomba kuwsilisha.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Matala na Lositete Karatu?
Supplementary Question 6
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Shule ya Msingi Malambeka, Shule ya Msingi za Mkomalilo A na Mkomalilo B, Shule ya Msingi ya Nachilo B zote zimebomoka na nyingine watoto sasa hivi wanakaa chini. Lini Serikali itaenda kurekebisha madarasa ya shule hizo ili watoto wasome?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza, nipokee kama ombi kutoka kwa Mheshimiwa Getere na sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI niwaelekeze wataalamu wetu waweze kufuatilia takwimu halisi za shule hizo na changamoto ambazo zimejitokeza, ambazo Mheshimiwa Mbunge ameziwasilisha, ili Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tuweze kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira bora ya kujifunzi ya wanafunzi wetu. Naomba kuwasilisha