Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 43 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 511 | 2026-06-04 |
Name
Twaha Said Mwakioja
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Primary Question
MHE. TWAHA S. MWAKIOJA aliuliza:-
Je, lini Serikali itakarabati madarasa chakavu na kujenga madarasa mapya katika Shule za Msingi Jimbo la Mkinga?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Twaha Said Mwakioja, Mbunge wa Jimbo la Mkinga kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kufanya ukarabati wa shule katika Wilaya ya Mkinga ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 mpaka kufikia mwaka 2025/2026, Serikali imepeleka jumla ya shilingi bilioni 2.78 katika Wilaya ya Mkinga kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mpya za msingi, madarasa 82 katika shule 35 chakavu za msingi na ukarabati wa shule tatu chakavu za msingi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 275.2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu, matundu ya vyoo 94 katika shule 19 za msingi katika Jimbo la Mkinga.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa na kukarabati shule za msingi chakavu nchini zikiwemo shule za Jimbo la Mkinga. Naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved