Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Twaha Said Mwakioja

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Primary Question

MHE. TWAHA S. MWAKIOJA aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati madarasa chakavu na kujenga madarasa mapya katika Shule za Msingi Jimbo la Mkinga?

Supplementary Question 1

MHE. TWAHA S. MWAKIOJA: Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Serikali kwa majibu mazuri na juhudi ambazo imezionesha kwa kipindi chote.

Mheshimiwa Spika, nimepata bahati ya kuzitembelea takribani shule zote za sekondari na msingi katika jimbo ninaloliongoza la Mkinga, kwa kweli hali ya shule hizi haiko vizuri hususan shule za msingi. Zipo shule zinavuja, zipo shule sakafu ni tifutifu kama vile uwanja wa mpira; na zipo kuta zinataka kuanguka.

Je, kutokana na hali hii, ni upi sasa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inaongeza fedha ambazo inazitenga ili kuondokana na adha hii; kwa sababu kuna baadhi ya madarasa nimeingia, watoto wanajitenga, hawa darasa la tano, hawa darasa la sita. Darasa moja wapo humo humo wanasoma pamoja. Ni upi mkakati wa Serikali kuongeza fedha ili kuhakikisha kwamba inaondokana na adha hii na kuweza kutoa elimu iliyo bora?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; nimwombe Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ikimpendeza tuongozane naye ili akaone adha ya shule na miundombinu iliyopo katika Jimbo la Mkinga. Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu maswali madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Twaha Said Mwaikoja, Mbunge wa Jimbo la Mkinga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tuliwasilisha katika bajeti katika Bunge lako hili Tukufu kwamba tunao mradi unaoitwa School Infrastructure Facelifting Programme (SIFA). Mradi huu unakwenda kuboresha shule hizi hasa zile kongwe na Bunge lako hili Tukufu lilipitisha bajeti ile na tutakwenda kuhakikisha kwamba tunaongeza fedha katika shule ambazo, kwanza ni chakavu na zile za muda mrefu na zile zenye mahitaji muhimu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tutahakikisha tunaongeza fedha katika maeneo yote aliyoyataja ili kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya elimu katika jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu ziara; Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tumeendelea kufanya ziara ambazo zinaongozwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu na tatatenga ratiba mimi na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kufika jimboni kuangalia miundombinu, siyo tu ya elimu hata maeneo mengine mbalimbali ili kuhakikisha kwamba ile azma ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuacha tabasamu kwa Watanzania inakwenda kutekelezwa. Naomba kuwasilisha.

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TWAHA S. MWAKIOJA aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati madarasa chakavu na kujenga madarasa mapya katika Shule za Msingi Jimbo la Mkinga?

Supplementary Question 2

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, ahsante, katika mkoa wangu wa Songwe kuna maboma mengi katika shule za msingi yalijengwa ni zaidi ya miaka kumi ambayo sasa nayo yameshapata uchakavu.

Sasa nataka kufahamu je, Serikali haioni kwa kuyaacha maboma hayo muda mrefu inawaumiza wananchi ambao walijitolea kipato chao kuweza kujenga maboma hayo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza Serikali inatoa pongezi kwa nguvu kubwa za wananchi, jitihada ambazo wananchi wameweka kujenga maboma hayo na pili, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI imeendelea kufanya tathmini, kuna yale maboma ambayo yanaweza yakamaliziwa ambayo bado yapo ndani ya ubora, lakini kuna yale maboma ambayo tayari yameshaharibika zaidi, hatutaweza kuyamalizia. Yale ambayo yapo ndani ya ubora tutaendelea kuyafanyia kazi, tutaendelea kutenga bajeti kuhakikisha kwamba tunayakamilisha, ili yaweze kutoa huduma katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyaainisha. Naomba kuwasilisha.

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. TWAHA S. MWAKIOJA aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati madarasa chakavu na kujenga madarasa mapya katika Shule za Msingi Jimbo la Mkinga?

Supplementary Question 3

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi; je, Serikali imeweka makakati gani kwenye bajeti hii ili ukarabati majengo ya shule za msingi ambayo yamechakaa sana ya shule kongwe? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kiswaga kama alivyoliuliza. Kama ambavyo nimekwishajibu kwenye majibu ya maswali madogo ya nyongeza, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tunao mradi mkakati wa SIFA; mradi huu unatakiwa kwenda kuboresha shule zote chakavu kongwe nchini, ili kuweza kutoa huduma bora na kuzirejesha kwa maana ya kwamba zianze kuendana na usasa ambao utatoa huduma bora ya elimu kwa wanafunzi wetu. Naomba kuwasilisha.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. TWAHA S. MWAKIOJA aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati madarasa chakavu na kujenga madarasa mapya katika Shule za Msingi Jimbo la Mkinga?

Supplementary Question 4

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Hai kuna shule nyingi chakavu na tumeshawasilisha andiko maalum TAMISEMI. Wakati tukiwa tunasubiria, hivi sasa mvua zinanyesha na maji yanaingia ndani, watoto wanashindwa kupata kuendelea na masomo. Shule ya Mkosaringe, Lyamungo, Shirimatunda, Rowu, Kisheri, Nkwamakuu, Tindigani, Waramu, Sereng na Shirimatunda.

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa dharura kuhakikisha shule hizi zinafanyiwa ukarabati ili watoto waweze kuendelea na masomo?

Name

Abdi Hija Mkasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Micheweni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa maana ya kwamba, anafuatilia, anatubana TAMISEMI kuhakikisha ya kwamba tunapeleka miundombinu stahiki na kwa wakati katika shule ambazo amezitaja.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza, jimbo hili lina shule kongwe kwa maana ya kwamba lilipata shule miaka ya nyuma sana. Kwa hiyo, wao walianza kupata miundombinu hii kwa kipindi cha miaka ya nyuma. Kwa hiyo, sasa hivi wameingia katika eneo la uchakavu na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tayari tumekwisha weka andiko, mipango mkakati kuhakikisha kwamba tunakwenda kuziboresha shule hizi ili ziweze kutoa huduma kusudiwa.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa pamoja na wanajimbo la Hai kwamba tutaendelea kupeleka fedha kuhakikisha kwamba tunakamilisha miundombinu hii ya shule na kuweza kutoa elimu kusudiwa. Naomba kuwasilisha.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TWAHA S. MWAKIOJA aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati madarasa chakavu na kujenga madarasa mapya katika Shule za Msingi Jimbo la Mkinga?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa shule za msingi za Nyanzwa, Ibumu, Ikula na Iramba ni shule chakavu mno katika wilaya yetu ya Kilolo, na niwapongeze Serikali kwamba ina mpango wa kuzikarabati shule kongwe zote ambazo zimechakaa sana.

Je, Serikali ipo tayari kutanzia katika wilaya yetu ya Kilolo kwa sababu zimechaka mno na ni magofu, watoto wanasoma kwenye mazingira magumu sana?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Dkt. Kabati wa Jimbo la Kilolo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimekwishatoa majibu ya Serikali kwamba tuna mpango makakati wa kupitia shule zote kongwe nchini na kuhakikisha tunaziboresha ili ziendane na usasa na kutoa huduma kusudiwa.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie wanakilolo wamekusikia na sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tumelichukua hili kuhakikisha kwamba katika kutenga vipaumbele na Jimbo la Kilolo tuweze kulitengea fedha na kwenda kufanya ukarabati wa shule hizo chakavu. Naomba kuwasilisha.