Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 43 Finance Wizara ya Fedha 515 2026-06-04

Name

William Kafiti Kafiti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. KAFITI W. KAFITI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha Kanuni za Bima za Kilimo ili kuongeza na kupatikana kwa kinga kwa wakulima na mazao mbalimbali?

Name

Laurent Deogratius Luswetula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kafiti William Kafiti, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utafiti kuhusu bima katika mnyororo wa kilimo yaani mazao, mifugo, misitu na uvuvi ili kwa pamoja na mambo mengine kuwa na kanuni zinazovutia uwekezaji katika bima ya kilimo na kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima ili kupata huduma za bima kwa urahisi na haraka. Ni mpango wa Serikali kukamilisha uandaaji wa kanuni hizi katika kipindi cha mwaka 2026/2027. Naomba kuwasilisha.