Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 19 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 219 | 2026-04-29 |
Name
Martha Nehemia Gwau
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA N. GWAU aliuliza:-
Je, lini Serikali itaweka Sheria ya Ugatuzi wa Madaraka kwa Serikali za Mitaa kama hatua ya kutekeleza Dira ya Taifa ya 2050?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Nehemia Gwau, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha Mfumo wa Ugatuzi kwa Serikali za Mitaa kama nyenzo muhimu ya kufanikisha maendeleo endelevu ya Taifa, hususan katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na tathmini mbalimbali, zilizofanyika Serikali imeandaa mapendekezo ya kutunga Sera ya Taifa ya Ugatuzi ya mwaka 2026 ambayo ipo katika hatua za maamuzi. Kupitia mapendekezo hayo, Serikali inalenga kuweka mfumo wa Kitaifa utakaoratibu kwa ufanisi utekelezaji wa ugatuzi nchini, kuziimarisha Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuongeza ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya maendeleo yao, pamoja na kuboresha mgawanyo wa madaraka, rasilimali na majukumu kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa sera hiyo unaweza kuambatana na mapitio ya baadhi ya sheria zilizopo au kutungwa kwa Sheria ya Ugatuzi pale itakapohitajika, kwa lengo la kuondoa changamoto za kiutendaji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo kuu ni kuhakikisha kuwa madaraka, rasilimali na maamuzi, vinashushwa kwa ufanisi zaidi katika ngazi za Serikali za Mitaa ili kuongeza tija, uwajibikaji, na kuchochea maendeleo ya wananchi kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya maeneo yao, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved