Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 220 2026-04-29

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge Jimbo la Chamazi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Charambe (Kilamba) ina urefu wa kilometa 1.3, ambapo hadi sasa mita 590 zimeboreshwa kwa kiwango cha zege na ziko katika hali nzuri kwa gharama ya shilingi milioni 676.9 huku meta 710 zilizobaki bado ni za changarawe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kuendelea kuijenga barabara hii kwa tabaka la zege kwa awamu na imeweka katika mpango na bajeti ya mwaka 2026/2027 kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa Temeke. Kiasi cha shilingi milioni 575.9 ambapo barabara hiyo itajengwa kwa urefu wa meta 710. Aidha, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu katika bajeti ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.