Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?
Supplementary Question 1
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mpango gani wa dharura kwa kuirekebisha barabara hiyo ili kuondoa adha kwa wajawazito?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuirekebisha barabara inayotoka Mashine ya Maji – Kanisani mpaka Zahanati hiyo ili kuwa barabara mbadala badala ya barabara hii?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii nimthibitishie Mheshimiwa Abdallah Chaurembo, kwamba tunatambua umuhimu wa barabara hii ikizingatia barabara hii inapita kwenye Zahanati ya Charambe (Kilamba). Kwa hiyo, inahitajika sana kwa huduma za afya kwa wananchi katika eneo hilo na ndiyo maana Serikali ilianza kwa kujenga kipande cha mita 590 kiwango cha zege na tunapanga kuendelea kujenga barabara hii kwa mita zilizobaki 710 kiwango cha zege kwa awamu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba suala hilo limechukuliwa kwa uzito unaotakiwa. Kwa maeneo ambayo hayapitiki kwa sasa, ninaomba nichukue nafasi hii nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke kwa kushirikiana na Meneja wa TATURA wa Wilaya ya Temeke na Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Dar es Salaam, wafike eneo la tukio kuona eneo ambalo halipitiki kabisa ili yafanyike matengenezo ya muda, wananchi waendelee kupita wakati tunasubiri matengenezo ya kudumu ya barabara hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara aliyoitaja ya Kanisani kuelekea kwenye zahanati hii, ni moja ya barabara ambazo sisi kama TAMISEMI tunazitambua na tunaziweka kwenye mpango kwa awamu kwa ajili ya kuzijenga ili ziweze kupitika vizuri. Kwa hiyo, tutaendelea kutekeleza miradi hiyo kwa awamu.
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni lini barabara ya Mbinga - Tanda - Masimeli hadi Miembeni itajengwa kwa kiwango cha changarawe?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka mpango wa kuhakikisha kwamba barabara zetu zile ambazo zinajengwa kwa kiwango cha udongo zinaanza kujengwa kwa kiwango cha changarawe ili kuanza kuboresha ubora wake, na pia kuhakikisha kwamba zinadumu kwa muda mrefu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini kwamba barabara hiyo ni moja ya barabara ambazo tutaendelea kuziewekea fedha kwenye bajeti zetu ili kuhakikisha kwamba zinaanza kujengwa kwa kiwango cha changarawe ili tuweze kuboresha zaidi huduma za usafiri kwa wananchi wa Mbinga Mjini.
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?
Supplementary Question 3
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii. Ni lini sasa barabara ya Mto Mbozi kwenda Tandali itajengwa? Ni kwa miaka mitatu sasa haijaguswa kabisa. Barabara hii iko katika Jimbo la Morogoro Kusini, ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge wa Morogoro Kusini amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na barabara hiyo na tulikwishawasiliana na Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Morogoro na walishawasilisha maombi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa Serikali iko kwenye taratibu za kutafuta fedha kwa ajili ya kwenda kufanya matengenezo ya barabara hizo, na barabara hizi nyingi zitatengenezwa baada ya mvua hizi ambazo zinaendelea kunyesha kukatika. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini kwamba Serikali hii sikivu inatambua, na italifanyia kazi.
Name
Agnesta Lambert Kaiza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?
Supplementary Question 4
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Ningependa kufahamu nini kauli ya Serikali kuhusiana na barabara inayotoka Segerea Mwisho kupitia kwa Makongoro Mahanga - Sekondari ya Ugombolwa - Zahanati ya Segerea kwa sababu ni mbovu na inasababisha wananchi wa Kata ya Segerea kushindwa kupata huduma. Nini kauli ya Serikali?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kauli ya Serikali ni kwamba Meneja wa TARURA wa Ilala afike kwenye barabara hiyo mapema iwezekanavyo afanye tathmini ya hicho kipande ambacho kina uharibifu mkubwa ambao unasababisha wananchi kushindwa kusafiri kutoka Segerea mwisho kwenda Zahanati ya Segerea ili kama inawezekana yafanyike matengenezo ya muda kuwezesha wananchi kupita wakati huo tunasubiri matengenezo yale makubwa ambayo yatafanyika baada ya mvua zinazoendelea kukatika.
Name
Mariam Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?
Supplementary Question 5
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la Sandali katika Jimbo la Temeke limekuwa sasa ni eneo la kibiashara hasa maeneo ya Vetinari. Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha Barabara ya Tarimo - Vetinari, Tarimo - BMK mpaka Kichangani katika Jimbo Kata ya Sandali? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, barabara alizozitaja Mheshimiwa Mbunge katika Jimbo la Temeke ni moja ya barabara ambazo zinahudumiwa kwanza na TARURA, lakini pia na DMDP awamu pili na Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba barabara zile zinaendelea kujengwa na kurekebishwa kwa awamu ili kuhakikisha kwamba zinatoa huduma zinazotakiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie mama yangu Mheshimiwa Mariam Kisangi kwamba barabara hizo ni kipaumbele cha Serikali na tutahakikisha tunaendelea kuzitengea fedha na kuzirekebisha ili maeneo hayo ya kibiashara, biashara ziweze kufanyika vizuri zaidi.
Name
Moshi Selemani Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanganyika
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Charambe Magengeni hadi Zahanati ya Kilamba ili kuondoa kero kwa Wagonjwa wanaoenda Hospitali ya Wilaya?
Supplementary Question 6
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali. Kata ya Ikola na Kata Isengule hazina mawasiliano kwa sababu ya kuvunjika madaraja; na Kata ya Sibwesa inayounganisha Kata ya Katuma ina hali kama hiyo. Je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kuzifanya hizo kata ziweze kuwa na mawasiliano?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, barabara zote ambazo zimeathiriwa na mafuriko na kukatika kwa maana ya madaraja, ma-culvert na barabara zenyewe, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tumeshatoa maelekezo kwa Mameneja wa TARURA mikoa yote na Mameneja wa TARURA wilaya zote kwamba kwanza wanatakiwa kufika kwenye maeneo hayo mapema kufanya tathmini na kuona yale ambayo yanaweza kutengenezwa yatengenezwe kwa haraka katika hali ya dharura ili yaweze kupitika wakati tunasubiri matengenezo makubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kakoso kwamba tutalifanyia kazi suala la madaraja hayo. Ninafahamu Tanganyika bado mvua zinaendelea kunyesha, kwa hiyo, yapo matengenezo ambayo yanawezekana na yapo ambayo yatasubiri mvua zikae sawa.