Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 221 2026-04-29

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Daraja linalounganisha Vijiji vya Wigelekelo Gumali, Masela na Barabara Kuu ya Mwigumbi Maswa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mto Tungu ni mto unaounganisha Kata ya Masela na Kata ya Bugarama katika Barabara ya Mwasayi – Masela - Wigelekelo inayohudumiwa na TARURA Wilaya ya Maswa yenye urefu wa kilomita 17.15. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini uliajiri Mkandarasi kwa ajili ya kujenga daraja la mawe kwa shilingi 87,220,000 ambapo kazi hiyo imeshakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali ilifanya ujenzi wa daraja dogo la mawe kwa gharama shilingi milioni 67.2 ambapo kazi hiyo imeshakamilika. Mwaka 2025/2026 Serikali imetenga shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa daraja katika Mto huo. Mchakato wa ununuzi kumpata Mkandarasi atakayetekeleza mradi huu unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, pindi ujenzi wa daraja katika Mto Tungu utakapokamilika utaunganisha vijiji vyote vitatu vya Mwasayi, Masela na Wigelekelo, ahsante.