Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Daraja linalounganisha Vijiji vya Wigelekelo Gumali, Masela na Barabara Kuu ya Mwigumbi Maswa?

Supplementary Question 1

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya ubovu wa barabara katika maeneo ambayo Mheshimiwa Ndaki ameyataja inafanana kabisa na hali ya ubovu wa barabara katika maeneo ya Mkinga, Wilaya ya Muheza na Tanga Mjini. Ni mkakati upi Serikali imeandaa kwa ajili ya kudhibiti hali hiyo katika maeneo yote hayo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kujenga kukarabati barabara zetu za TARURA kote nchini. Hata hivyo, tunafahamu katika kipindi hiki cha msimu wa mvua barabara nyingi za halmashauri zetu zikiwepo Halmashauri ya Maswa, Mkinga, Muheza na maeneo mengi kote nchini zimeharibiwa na mvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ambazo Serikali imechukua, moja ni kuendelea na matengenezo ya barabara, madaraja na ma-culvert kwa dharura ili kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea. Pili, tumeendelea kufanya tathmini ya gharama ya fedha inayohitajika kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo zilizoathiriwa na mvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mkakati wa Serikali uko thabiti kwamba tunaweka utaratibu mzuri baada ya mvua kukatika tutakwenda kuanza kutengeneza barabara hizi, madaraja na ma-culvert kwa awamu ili kurejesha hali ya usafiri katika hali yake ya kawaida.

Name

Hemed Sumry Haidary

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Daraja linalounganisha Vijiji vya Wigelekelo Gumali, Masela na Barabara Kuu ya Mwigumbi Maswa?

Supplementary Question 2

MHE. HAIDARY H. SUMRY: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Nswima ambayo inaunganisha majimbo matatu katika Mkoa wa Katavi; Jimbo la Mpanda Mjini, Jimbo la Nsimbo na Jimbo la Tanganyika katika eneo la Mtapenda na Kasokola imekatika kabisa. Nini kauli ya Serikali kurudisha mawasiliano katika eneo hili? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kumwelekeza Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Katavi, lakini pia wa Wilaya ya Mpanda, Nsimbo pamoja na Tanganyika wafike katika eneo hilo lililokatika wafanye tathmini na yafanyike matengenezo yatakayowezesha barabara kuendelea kutumika wakati tunasubiri matengenezo makubwa na huduma katika barabara hiyo.

Name

Morris Joseph Makoi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Daraja linalounganisha Vijiji vya Wigelekelo Gumali, Masela na Barabara Kuu ya Mwigumbi Maswa?

Supplementary Question 3

MHE. MORRIS J. MAKOI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Mawasiliano kati ya Kata ya Kirima na Kindi yamekatika tangu mwezi wa Nane mwaka 2025. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha za dharura kurejesha daraja la kata hizo mbili ili mawasiliano yaendelee?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea maombi ya Mheshimiwa Makoi, Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Moshi na Mkoa Kilimanjaro na hivi sasa Serikali inaendelea na taratibu za kupata fedha ili kwenda kufanya matengenezo ya barabara hizo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba suala hilo litatekelezwa.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Daraja linalounganisha Vijiji vya Wigelekelo Gumali, Masela na Barabara Kuu ya Mwigumbi Maswa?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Ni lini barabara ya kutoka Ilula kwenda Image mpaka Igumu itajengwa kwa sababu wananchi wamesubiri kwa muda mrefu, na sasa hivi magari yanakwama, nyanya zinaozea barabarani.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Ilula na ambayo inapita katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja katika Jimbo la Kilolo ni moja ya barabara ambazo ni kipaumbele na ziko kwenye mtandao wa barabara za TARURA katika Wilaya ya Kilolo na Serikali inaendelea kuandaa fedha, lakini tunaendelea kusubiri hali ya hewa ya mvua zipungue ili tuanze matengenezo kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati kwamba barabara hiyo itapewa kipaumbele.