Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 19 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 225 | 2026-04-29 |
Name
Amina Mussa Mkumba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kibiti
Primary Question
MHE. AMINA M. MKUMBA aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA katika Jimbo la Kibiti?
Name
Wanu Hafidh Ameir
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Amina Mussa Mkumba, Mbunge wa Kibiti, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kibiti ni miongoni mwa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi 65 vinavyoendelea kujengwa katika wilaya 64 na Mkoa mmoja wa Songwe. Ujenzi huo unafanyika katika wilaya au mkoa ambao hauna Chuo cha VETA.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kibiti ambacho kinatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2026. Hadi sasa Serikali imeshatumia jumla ya shilingi bilioni 1.1 kati ya shilingi bilioni 1.6 zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza. Mpaka sasa ujenzi huo umefikia 69% ya utekelezaji wake.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved