Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Charles Mhando Njama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. AMINA M. MKUMBA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA katika Jimbo la Kibiti?

Supplementary Question 1

MHE. CHARLES M. NJAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Chuo cha Ualimu Korogwe ni chuo kikongwe na cha muda mrefu, lakini hadi leo hakina uzio. Je, yupo tayari kwenda kutembelea chuo kile na kuanza ujenzi wa uzio katika chuo cha ualimu Korogwe?

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze kwa kufuatilia maendeleo ya Chuo cha Ualimu cha Korogwe na nimwambie kwamba nipo tayari kwenda kutembelea chuo hicho na kuona namna gani tutaweza kusaidia kujenga uzio wa chuo hicho.