Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 19 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 227 | 2026-04-29 |
Name
Anton Albert Mwantona
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rungwe
Primary Question
MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: -
Je, lini Mradi wa Maji katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, utaanza kutekelezwa?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Mpandapanda kilichopo Kata ya Kiwira kinapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi uliotekelezwa kijijini hapo mwaka 2021/2022 kupitia fedha za UVIKO 19. Kiasi cha shilingi milioni 306.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuboresha zaidi huduma ya maji Kata ya Kiwira, Serikali imekamilisha usanifu wa mradi mkubwa utakaotumia chanzo cha maji cha Mto Katalifu unaolenga kunufaisha vijiji vyote vinne vya Mpandapanda, Kikota, Ilundo na Ibula. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanza utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 5.2.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved