Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, utaanza kutekelezwa?

Supplementary Question 1

MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nakushukuru sana kwa majibu ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mradi wa Masoko, Awamu ya Pili, ambao ulikuwa unahudumia Vijiji vya Irima, Ndulu pamoja na Omburi. Mradi huu ulianza, lakini kwa bahati mbaya sana mkandarasi ameondoka kwa sababu ya kutolipwa fedha za awali. Je, ni lini mtamlipa mkandarasi fedha za awali, ili mradi huu uendelee kutekelezwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kuna miradi sita katika Jimbo la Rungwe, ambayo imesimama kutokana na wakandarasi hajalipwa fedha zao. Ninaomba nijue Serikali inakwenda kuwalipa lini wakandarasi fedha hizo, ili miradi iweze kuendelea?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, ninampongeza sana Mheshimiwa Anton Albert Mwantona kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuwasemea wananchi wa Rungwe, ili wapate huduma ya majisafi na salama, lakini yaliyo toshelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na yote, upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama Jimbo la Rungwe kwa sasa ni 76.5%, lakini pia, pamoja na miradi ambayo amesema iko sita, ndani ya Jimbo la Rungwe tunayo miradi 10. Kuna uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita wa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 12.9 kwa hiyo, ninamtoa hofu katika eneo hilo, sisi tumejizatiti, tumejipanga kwenda kuhakikisha kwamba, miradi yote ambayo imeanza tunaenda kuhakikisha inakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi kubwa ambayo sasa tunaifanya ni kuangalia vipaumbele. Tunapoangalia vipaumbele vya Kitaifa, tunapokuja kwenye jimbo, tunaangalia mradi upi tuanzenao, ukamilike, utoe matokeo, halafu tufuate mradi mwingine kwa hiyo, tutakaa Mheshimiwa Mbunge, ili tuweze kupanga vipaumbele vya jimbo lake na ili tuweze kuweka msukumo wa kupeleka fedha miradi ikamilike kwa hatua kwa sababu, hatuwezi kukamilisha kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, suala la Mradi wa Masoko, Awamu ya Pili, mradi huu tunatambua kwamba ni msingi wa uchumi wa eneo la Rungwe. Tunauchukua kwa uzito mkubwa sana. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea kuandaa malipo kwa ajili ya mkandarasi ili apatiwe hizo fedha akaanze huo mradi haraka sana. Lengo ni kwamba, wananchi wa Rungwe wapate huduma ya majisafi na salama. Tunavyo vipaumbele hivyo, kwa ajili ya wananchi wake.

Name

Kakulu Burchard Kakulu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, utaanza kutekelezwa?

Supplementary Question 2

MHE. KAKULU B. KAKULU: Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu linahusiana na Jimbo langu la Mbagala. Ziko kata kadhaa ambazo zilikuwa na miradi ambayo wananchi walianzisha wenyewe na wakati ikiwa mikononi mwa wananchi, imefanya kazi nzuri sana. Baada ya kuchukuliwa na DAWASA kumekuwa na changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya Kata ya Kijichi, Kata ya Mbagala na Kata ya Mbagala Kuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba Mheshimiwa Naibu Waziri atupe hakikisho, je, Serikali iko tayari kuirejesha hiyo miradi kwa wananchi ili tui-manage wenyewe na tuendelee kupata maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nisiwe mwongo, kwa usimamizi wa miradi ya maji na huduma ya maji tunaenda sambamba na maelekezo ya sera yetu. Sera yetu inaturuhusu, kwanza Serikali kusimamia miundombinu na pia, kuhakikisha maji yanatoka na ni salama (secure of water), lakini pia, yawe toshelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muktadha huo, tunapoongelea maji, ni usalama wa Taifa, tunaangalia namna ambavyo tunaweza kushirikisha wananchi kwenye ownership ya kujua mradi ni wa kwao, lakini usimamizi wa mradi bado utabaki katika mamlaka ambayo imetamkwa kwenye sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninamtoa hofu, kama kuna jambo na changamoto za usimamizi wa miradi hiyo, sisi tutatuma timu yetu, itaenda kufanya tathmini na kuangalia wapi kuna tatizo ili tuweze kutatua, lakini siyo kurudi kule ambako hatuwezi kufika tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii ina sensitivity yake, kwa hiyo, tukisema kwamba, kwa mujibu wa Sheria yetu Na. 5 ya Mwaka 2019, ambayo ndiyo ilianzisha Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira, ndiyo yenye jukumu la kisheria la kusimamia na kuendeleza huduma za maji vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwenye hili naomba nisiseme uongo kwamba tutawarejeshea wananchi, hilo tutakuwa tunavunja sheria. Kikubwa ni kwamba tutawashirikisha wananchi kwenye kuelewa na kuwa na upana wa kujua nini maana ya miradi ya maji na nani anatakiwa kusimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika naomba kuwasilisha.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, utaanza kutekelezwa?

Supplementary Question 3

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza, ninaipongeza Serikali kwa kazi kubwa iliyoifanya kuhakikisha Wilaya ya Karatu inapata majisafi na ya uhakika. Natambua kesho Mheshimiwa anaenda kufanya uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Joba Chibumbe Chani, pale Karatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba, kuna Vijiji vya Apakitete na Tahamo katika Kata ya Mbulumbulu, Wilayani Karatu, pamefanyika majaribio kadhaa ya kuchimba maji bila mafanikio kwa hiyo, inahitajika fedha kwa ajili ya kufanya utafiti maeneo ya mbali kama kuna maji ili waweze kuchimba. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha hizo kwa ajili ya utafiti?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa Serikali inapochimba visima inafanya majaribio. Sehemu nyingi tumepata changamoto. Tunachokifanya ni kwamba tunatafuta miradi iliyoko karibu na vijiji husika, tunafanya stadi, tunafanya usanifu na tunafanya cost benefit analysis ya kuangalia eneo lingine ambapo tunaweza tukachimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumeweka mpango mzuri na tunauingiza kwenye Mpango huu wa Bajeti wa Mwaka 2026/2027, ili sasa tupeleke fedha, Serikali ikaangalie eneo lingine la kuchimba ama kutengeneza mradi uliopo karibu na vijiji hivyo, uwekewe miundombinu ya kufikisha huduma ya majisafi na salama katika vijiji ambavyo havina maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, lengo ni jema kabisa na ninakushukuru sana kwa swali hili zuri kabisa ambalo linalenga kuwasaidia wananchi wake, na kweli, kesho ni juhudi zake pia, pamoja na Wabunge wenzake katika eneo ambalo tunaenda kuzindua mradi huo ambao tunaamini kwamba atakuwa ni game changer katika eneo la Karatu, asante sana.