Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 19 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 228 | 2026-04-29 |
Name
Marirta Gido Kivunge
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIRTA G. KIVUNGE aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Miradi ya Maji iliyosimama kwenye Halmashauri za Wilaya ya Meru, Longido na Monduli?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inakamilisha utekelezaji wa miradi ya maji yote inayoendelea na ile iliyosimama kote nchini, ikiwemo miradi sita inayoendelea katika Halmashauri za Wilaya za Meru, Longido na Monduli. Miongoni mwa miradi inayoendelea katika wilaya hizo ni pamoja na Mradi wa Maji Kikatiti, Samaria; Mradi wa Maji Kata ya Uwiro iliyopo Wilaya ya Meru; Miradi ya Maji Tingatinga na Ketumbeine, Wilaya ya Longido, sambamba na mradi wa maji unaolenga kunufaisha vijiji 13 vya Wilaya ya Monduli.
Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hiyo yote kwa pamoja inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 38.7, ambapo hadi mwezi Machi, 2026 zaidi ya shilingi bilioni 5.8 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji. Mpango wa Serikali ni kuendelea kutoa kipaumbele cha kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kadiri zinavyopatikana, ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved