Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 19 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 230 | 2026-04-29 |
Name
Yustina Arcadius Rahhi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua mashamba yaliyokuwa ya ngano nchini ili kuweza kukidhi mahitaji ya ngano nchini?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeandaa mpango wa uendelezaji wa mashamba ya kilimo ikiwemo yale yaliyokuwa ya NAFCO yanayojumuisha mashamba ya ngano ya Basutu. Kupitia mpango huo, miongoni mwa hatua zilizopangwa ni kutafuta wawekezaji mahiri (strategic investors) wenye uwezo wa kuendeleza mashamba hayo kwa tija.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali imepanga kufanya ufuatiliaji wa wawekezaji waliobinafsishwa mashamba yao ya Ngano ya Setchet, Gidagamowd na Murjanda chini ya kampuni ya Ngano Limited ili kubainisha changamoto na kutoa mapendekezo ya kisera yatakayowezesha uendelezaji endelevu wa mashamba hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji wa ngano nchini kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo kubainisha maeneo mapya ya uzalishaji.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved