Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 19 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 231 | 2026-04-29 |
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza:-
Je, lini barabara ya Mlowo – Kamsamba itaanza kujengwa kwa kuwa ni zaidi ya mwaka tangu mkandarasi asaini mkataba?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mlowo - Kamsamba yenye urefu wa kilomita130 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo Serikali tayari imekamilisha ujenzi wa Daraja la Momba na Daraja la Mpapa. Aidha, Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa kilometa tano kuanzia Mlowo kuelekea Kamsamba na kilometa nyingine tano kuanzia Kamsamba kuelekea Mlowo amepatikana, ambapo taratibu za malipo ya awali ya kumwezesha kuanza kazi, zinaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sehemu zilizobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved