Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 19 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 232 2026-04-29

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASIA A. HALAMGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanzisha kiwanda cha kuchakata mazao katika Jimbo la Hanang?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Asia Abdulkarim Halamga, Mbunge wa Jimbo la Hanang kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Hanang huzalisha mazao mbalimbali ikiwemo mahindi, alizeti, ngano, dengu na mbaazi. Mwaka 2024/2025 wilaya hii ilizalisha mahindi tani 130,980.3, alizeti tani 30,732.3, mbaazi tani 19,173.6, dengu tani 30,960.2, na ngano tani 12,600. Wilaya hii ina jumla ya viwanda 1,226, ambapo kati ya hivyo viwanda vya kuchakata mahindi ni 346 na viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti ni 69. Viwanda 811 vinavyobaki ni vya matofali, mbao, kushona na mikate.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Kilimo pamoja na Mkoa wa Manyara tunaendelea kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vya mazao ya dengu, ngano na mbaazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.