Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 192 2026-04-27

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja ya kutenga sehemu ndogo ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya samani za ofisi na ufuatiliaji wa miradi ya Mfuko huo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Jimbo la Lulindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo huchangia shughuli na miradi ya maendeleo inayobuniwa na kuibuliwa na wananchi kupitia mpango wa fursa na vikwazo na kuidhinishwa na halmashauri. Katika kutekeleza azma hii, mwaka 2009 Bunge lako lilipitisha Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo Sura ya 96 ambayo imeanzisha Mfuko pamoja na Kamati ya kuchochea maendeleo ya jimbo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kifungu cha 8 na 19 cha Sheria hiyo kinabainisha aina ya miradi inayoweza kugharamiwa chini ya sheria hii. Miradi hiyo ni pamoja na miradi ya kijamii ambayo ni lazima iwe na manufaa kwa sehemu kubwa ya wakazi wa jimbo husika. Miradi ya maendeleo, inaweza kujumuisha gharama za utafiti, upangaji, usanifu au mchango wa kitaalamu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi; miradi ya miundombinu na huduma za jamii mfano ujenzi wa shule, zahanati, barabara ndogo, miradi ya maji, na miradi ya kilimo cha pamoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sheria hiyo inaruhusu kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ufuatiliaji wa miradi, lakini siyo kwa matumizi ya samani au gharama za kawaida za ofisi. Kwa msingi huo, halmashauri zinaweza kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo kutekeleza jukumu la ufuatiliaji wa miradi, lakini siyo kwa matumizi ya samani. Ahsante.