Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:- Je, Serikali haioni haja ya kutenga sehemu ndogo ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya samani za ofisi na ufuatiliaji wa miradi ya Mfuko huo?

Supplementary Question 1

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nifahamu je, ni kiasi gani kinachoruhusiwa kutumika kwa ajili ya ufuatiliaji wa samani hizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi kumekuwa na changamoto, unavyokwenda kuwaambia halmashauri kwamba waweze kutoa kiasi cha fedha kwa ajili ya samani za ofisi kwenye Mfuko wa Jimbo zinakuwa hazitoki. Je, Serikali haioni kuwa kuna sababu sasa ya kuipa hadhi Ofisi ya Mbunge kwa kuhakikisha kwamba inatoa fedha maalumu kabisa kwa ajili ya samani (viti, pamoja na meza) ambapo wakati wageni au watu wanaokuja kuleta changamoto zao pale wanaweza hata kukaa katika viti hivyo? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mfuko wa Jimbo ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria Sura 96 na Vifungu vile cha 8 na 19 kimeeleza vizuri kwamba shughuli zipi zinatakiwa kutekelezwa kwa Mfuko wa Jimbo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mchungahela, kwanza tunafahamu kwamba Mfuko huu unatekeleza shughuli za miradi ambayo iko ndani ya halmashauri iliyoibuliwa na wananchi na inaruhusiwa kutumia sehemu kidogo ya fedha hizo kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastani wa asilimia mbili hadi tano ya fedha ile inaweza ikatumika kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ambayo imedhaminiwa na Mfuko wa Jimbo.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili, Mfuko wa Jimbo hauruhusiwi kutumika kwenye samani za ofisi za Waheshimiwa Wabunge. Tunavyo vyanzo vingine ambavyo vinaweza vikatumika kuboresha Ofisi za Waheshimiwa Wabunge, na tunatambua umuhimu wa Ofisi za Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mchungahela, ikiwa kuna uhitaji wa samani katika ofisi ya Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine, tutaona utaratibu mzuri ambao Serikali imeuweka kwa ajili ya kuhakikisha Waheshimiwa Wabunge wana ofisi nzuri kwa matumizi yao. (Makofi)

Name

Ibrahim Mohamed Shayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:- Je, Serikali haioni haja ya kutenga sehemu ndogo ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya samani za ofisi na ufuatiliaji wa miradi ya Mfuko huo?

Supplementary Question 2

MHE. IBRAHIM M. SHAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Moshi Mjini kuna madaraja mawili; daraja la kwanza lipo Kata ya Ng’ambo na daraja la pili lipo Kata ya Mji Mpya. Madaraja yale kutokana na mvua hizi, ni mabovu sana. Je, ni lini Serikali itakwenda kuyarekebisha madaraja haya ili wananchi wale wawe salama? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Shayo, Mbunge wa Moshi Mjini kwamba Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na madaraja na kuyatengeneza mara kwa mara. Ninafahamu Mheshimiwa Mbunge ana changamoto ya Daraja la Kata ya Ng’ambo ambalo limekatika siku chache zilizopita na kuathiri mawasiliano kutoka kata hiyo kwenda kata za jirani. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali hii itafuatilia kuhakikisha kwamba tunafanya matengenezo mapema iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kumwelekeza Meneja wa TARURA, Wilaya ya Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro wafike eneo la site wafanye tathmini mapema iwezekanavyo ili tupate fedha za dharura kwa ajili ya kurekebisha hali hiyo. (Makofi)