Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 193 2026-04-27

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:-

Je, Serikali imejipangaje kumaliza tatizo la matundu ya vyoo katika halmashauri nchini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya upungufu wa vyoo katika baadhi ya shule za msingi na sekondari nchini. Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya elimu msingi ya mwaka 2025 uwiano wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi wa shule za msingi ni 1:46 (wavulana) na 1:42 (wasichana) na sekondari uwiano ni 1:27 (wavulana) na 1:25 (wasichana).

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutenga fedha na kujenga matundu ya vyoo kila mwaka, ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi bilioni 12.87 zilitumika kujenga matundu 6,283. Katika mwaka wa fedha 2025/2026 hadi Aprili, 2026 kiasi cha shilingi bilioni 5.42 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 6,283.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha katika bajeti kila mwaka ili kutatua changamoto za matundu ya vyoo nchini, ahsante.