Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 195 2026-04-27

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko la Kisasa la Machinga katika Jimbo la Tabora Mjini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga, Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Soko la Machinga katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora upo katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2025 - 2030) wa Halmashauri hiyo. Ujenzi huo umepangwa kuanza katika Mwaka wa Fedha 2027/2028.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa 2026/2027 Halmashauri imetenga shilingi milioni 150 kupitia mapato ya ndani, ili kuanza maandalizi ya nyaraka za miradi ya kimkakati ikiwemo soko hilo. Nyaraka zitakazoondaliwa na upembuzi yakinifu wa miradi huo utafanyika. Baada ya halmashauri kukamilisha maandalizi na upembuzi yakinifu wa mradi huo, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, itafanya mapitio ya maandiko dhana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora katika utekelezaji wa ujenzi.