Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 196 2026-04-27

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza: -

Je, lini barabara ya Hedaru - Mamba Vunta yenye Km 42.44 itaboreshwa ili kuokoa uchumi wa Wananchi wa Kata ya Mamba Vunta?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikihudumia Barabara ya Hedaru - Vunta - Myamba yenye urefu wa kilometa 42.44 (Hedaru - Mamba Vunta) kwa vipindi tofauti kwa kuijenga na kuifanyia matengenezo mbalimbali tangu mwaka 2020/2021 hadi 2024/2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu zenye kona hatarishi 13 zilizoko katika mlima wa Kidenge zilifanyiwa matengenezo makubwa. Matengenezo hayo ni kujengwa kwa kiwango cha zege kwa kilomita 2.04, kujenga makalavati 18, drifti nane, daraja moja, ujenzi wa mifereji mita 1,800, kuchonga barabara kilometa 40, kuweka changarawe kilomita 15 na ujenzi wa kingo kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa barabara kwa jumla ya shilingi bilioni 2.73.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2026/2027, Serikali imeweka katika mipango yake bajeti ya shilingi milioni 102 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya kawaida katika barabara ili kuhakikisha inaendelea kupitika wakati wote, ahsante.