Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 18 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 204 | 2026-04-28 |
Name
Anna Richard Lupembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-
Je, lini Serikali itakarabati Shule ya Msingi Mtapenda Kata ya Mtapenda – Nsimbo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Msingi Mtapenda ilijengwa mwaka 1970, na hivyo ni chakavu na inahitaji ukarabati. Katika mipango ya ukarabati wa shule chakavu, Serikali katika mwaka 2021/2022 ilifanya tathmini na kubaini jumla ya shule 10,595 chakavu kote nchini ambapo jumla ya shilingi trilioni 2.8 zinahitajika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kuptia Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, imeandaa andiko la mradi unaoitwa SIFA yaani (School Infrastructure Facelifting Programme) na kuwasilisha Wizara ya Mipango na Uwekezaji ili kuwezesha upatikanaji wa fedha za kufanyia ukarabati wa shule zote kongwe za awali, msingi na Sekondari nchini ikiwemo Shule ya Msingi Mtapenda, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved