Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 18 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 207 2026-04-28

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza kada ambazo hazipo kwenye orodha ya kada za Sekretarieti ya Ajira kwa kuwa zinafundishwa vyuoni?

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuwa vyuo Vikuu na vyuo vya elimu ya juu hutoa mafunzo ya programu za fani mbalimbali kwa vijana ambao wanaweza kuajiriwa katika utumishi wa umma au katika sekta binafsi nchini. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma husimamia taratibu za ajira kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa katika miundo ya maendeleo ya utumishi ya kada zilizo chini ya Wizara mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuwa baadhi ya fani zinazofundishwa katika vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu hazijawekewa utaratibu wa ajira kama fani nyingine ambazo wahitimu wake wanaajiriwa katika utumishi wa umma au sekta binafsi. Hivyo, tunaelekeza vyuo kuwasiliana na Serikali mapema kabla ya kuanzisha programu za fani ili kuwezesha utengenezaji wa mifumo ya ajira hizo.