Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 18 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 208 2026-04-28

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Primary Question

MHE. NAPE M. NNAUYE aliuliza: -

Je, Serikali ipo tayari kuweka wazi mpangokazi wa mwelekeo wa mazungumzo juu ya Mradi wa LNG - Lindi kwa kuwa umechukua muda mrefu?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nishati ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, Mbunge wa Jimbo la Mtama, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali na wawekezaji wa mradi wa LNG wapo katika hatua ya mwisho ya majadiliano hususani kwenye masuala ya kisheria ili kuwezesha usainishaji wa mikataba na makubaliano na hatimaye utekelezaji wa mradi kuanza. Aidha, majadiliano yatakapokamilika, rasimu za mikataba hiyo zitawasilishwa Serikalini kwa ajili ya mapitio na kupata ridhaa kabla ya kusainiwa rasmi ili kuwezesha utekelezaji wa Mradi kuanza mara moja.