Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Primary Question
MHE. NAPE M. NNAUYE aliuliza: - Je, Serikali ipo tayari kuweka wazi mpangokazi wa mwelekeo wa mazungumzo juu ya Mradi wa LNG - Lindi kwa kuwa umechukua muda mrefu?
Supplementary Question 1
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Pamoja na maelezo ya Serikali ya mara kwa mara juu ya mradi huu mkubwa nchini na tukizingatia kuwa wakati Mheshimiwa Waziri wa Nishati anahitimisha bajeti yake hapa wiki iliyopita, aliahidi Bungeni hapa kwamba wiki hii wakuu wa hizi kampuni kubwa ambazo zinawekeza kwenye huu mradi watakuwepo hapa nchini kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya jambo hili. Ahadi hii imefikia wapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwenye miradi mikubwa kama hii maandalizi ya wananchi na hasa wa level ya chini katika kushiriki kwenye hii miradi mara nyingi inakuwa ni jambo ambalo lina changamoto kubwa kama Serikali haitaingiza mkono wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inampango gani wa kufanya maandalizi ya kutosha kwa wananchi hasa wa kawaida na hasa wa maeneo ya Lindi na Mtwara ambako mradi huu unatekelezeka ili kuwaandaa kuzijua na kushiriki fursa zinazotokana na uwekezaji huu mkubwa katika nchi yetu? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, Mbunge wa Mtama kwa maswali ya msingi na kulifuatilia jambo hili. Ukweli ni kwamba amekuwa akilipigania hili kutaka lifike mwisho kwa sababu lina manufaa makubwa kwa Taifa, hususan katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, nimpongeze sana kwa hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mheshimiwa Nape kwamba leo tunavyozungumza, Waziri wa Nishati pamoja na timu ya Wizara wanakutana na wawekezaji wa Kimataifa kwa maana ya IOC’s, wameshawasili hapa nchini. Ninavyozungumza hivi, ni kwamba jioni ya leo utaona picha zitakavyopigwa kwa sababu ni sehemu ya huo mjadala kuhakikisha kwamba wanafanya majadiliano na jambo hili linakwisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu mpango wa Serikali ni kwamba moja ya mpango wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha; moja, zitatolewa kozi maalum kwenye vyuo vyetu vya VETA kwa ajili ya kuwanufaisha wale wananchi ambao kupitia ujuzi watakaoupata watautumia ule ujuzi ili wanufaike na fursa zote zinazotokana na mradi wa LNG.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kuna component ya local content ambayo wananchi wa kawaida katika maeneo hayo watanufaika. Kwa hiyo, niseme mradi huu kwa sababu phase ya kwanza, ni karibu miaka mitano, lakini wananchi watanufaika zaidi kwa sababu Serikali imejipanga kuhakikisha kila kilichopo hapa nchini wananufaika moja kwa moja. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved