Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 18 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 209 2026-04-28

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Primary Question

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Umeme katika Shule za Sekondari, Msingi na Taasisi zote za Wilaya ya Karagwe?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nishati ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa, Mbunge wa Jimbo la Karagwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Karagwe jumla ya vitongoji 334 kati ya vitongoji 612 vimepatiwa umeme hadi sasa na Shule za Msingi 109, Shule za Sekondari 37 za vitongoji hivyo zimeunganishiwa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji 61 ambapo kipaumbele ni kufikisha umeme katika taasisi zinazohudumia jamii zikiwemo shule, vituo vya afya, pampu za maji na nyumba za ibada. Aidha, Serikali itaendelea kuziunganishia umeme taasisi katika vitongoji 217 vya Wilaya ya Karagwe vilivyosalia kupitia miradi mbalimbali ya umeme inayotarajia kuanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027.