Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Primary Question
MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Umeme katika Shule za Sekondari, Msingi na Taasisi zote za Wilaya ya Karagwe?
Supplementary Question 1
MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Mamlaka ya Kayanga na Omurushaka yapo maeneo ambayo pamoja na kuwa kwenye Mamlaka ya Mji, kiuhalisia ni vijijini na maeneo haya gharama za kufunga umeme ni shilingi 320,000 kama mwananchi anafunga umeme kutoka kwa jirani, yaani bila nguzo. Kwa hiyo, shilingi 320,000 waya pamoja na mita, lakini akilazimika kulipia gharama ya nguzo pamoja na mita ni shilingi 515,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tu mfano, kwa Kata ya Ihanda maeneo kwa mfano Kantikimo, Chamezi, Katunguru, Ruswa, Nyakakiri, Omukagera, na hata Kata ya Bugene maeneo ya Bujuruga Centre ya Ibombo, Ruzinga eneo la Mkiziku hata Kayanga maeneo ya Miti wananchi wanalipa gharama kubwa. Swali langu, je, Serikali ipo tayari kufunga umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama maeneo mengine ya vijijini? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nami pia nimpongeze vile vile Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa, Mbunge wa Karagwe kwa swali zuri la msingi ambalo lina maslahi makubwa kwa wananchi wake lakini ni kwa Taifa zima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu jambo moja, wiki iliyopita Waziri wa Nishati, Komredi Deo Ndejembi akiwa kwenye podium hii alishatolea maelekezo kwamba moja ya mpango wa Serikali ni mpango ule ambao unahusisha maeneo ya miji, lakini yana vijiji (Peri-urban plans) na katika ule mradi Mheshimiwa Waziri hapa alishasema wameuchukua na aliwataka REA pamoja na TANESCO kukaa pamoja na kuainisha yale maeneo ambayo yako ndani ya miji lakini yana vijiji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, yeye mwenyewe Mheshimiwa Waziri amenithibitisha niwaambie Waheshimiwa Wabunge, hivi karibuni watu wa REA wataanza kuwapigia wananchi pamoja na Waheshimiwa Wabunge na watu wa TANESCO kwa jambo moja tu la kuainisha yale maeneo ili yaweze kufanyiwa tathmini na yaweze kuingizwa katika mpango wa utekelezaji kuanzia mwaka huu fedha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved