Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 18 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 210 | 2026-04-28 |
Name
Kassimu Amari Mbaraka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanga Mjini
Primary Question
MHE. KASSIMU A. MBARAKA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa Barabara ya Kiomoni, Pande, Mjesani hadi Muheza inayounganisha Wilaya ya Tanga na Muheza utaanza?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kassimu Amari Mbaraka, Mbunge wa Tanga Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kiomoni, Pande, Mjesani ni sehemu ya barabara ya Mkoa ya Mlingano – Mjesani - Pande hadi Kiomoni yenye urefu wa kilometa 39.5 na inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Kazi ya upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara hii kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2027. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved