Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 18 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 211 | 2026-04-28 |
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kilometa 23 kutoka Mlandizi hadi Ruvu Station (SGR) kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mlandizi hadi Stesheni ya SGR kilometa 23 inaunganisha barabara ya Morogoro (TANZAM) katika eneo la Mlandizi na Reli ya SGR katika Stesheni ya Ruvu. Kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, tayari Serikali imesaini mkataba na Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hiyo, na kwa sasa, Serikali inaendelea na taratibu za malipo ya awali ili kumwezesha Mkandarasi kuanza kazi za ujenzi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved