Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kilometa 23 kutoka Mlandizi hadi Ruvu Station (SGR) kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inaungana na Barabara ya Tanga – Segera - Dar es Salaam na Barabara ya Dar es Salaam – Segera – Moshi - Arusha ambayo kwa sasa imezidiwa na magari mengi hasa malori kutoka Bandari ya Tanga. Je, ni upi mkakati wa upanuzi wa barabara hii pamoja na barabara ambayo Mheshimiwa Hawa ameuliza?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba hizi barabara nyingi zimechoka, lakini pia zimekuwa finyu. Mkakati ambao tunao, kwanza kuanzia Mlandizi hadi Chalinze ni kuweka expressway ambazo zitakuwa ni njia nne, lakini kuanzia Mlandizi kwenda Segera tulishafanya usanifu ili kuweza kuongeza upana wa hiyo barabara na kuweza kwenda na upana wa barabara ambazo sasa hivi zinajengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua ni barabara ambayo imejengwa muda mrefu, na kwa kweli ni finyu hasa kulingana na kazi kubwa ambayo imefanyika kuipanua Bandari ya Tanga na kuongeza mizigo na kufanya magari yawe mengi. Kwa hiyo, tuko na mpango wa kuweza kuipanua hiyo barabara.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved