Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 17 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 201 2026-04-27

Name

Cosmas Mtesigwa Bulala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwimba

Primary Question

MHE. COSMAS M. BULALA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao katika Kijiji cha Hungumalwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuimarisha miundombinu ya uhifadhi wa chakula nchini, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali ilikamilisha ujenzi wa ghala 28 katika Mkoa wa Ruvuma yenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 28,000. Lengo ni kuhakikisha upotevu wa mazao ili kuimarisha usalama wa chakula nchini unapungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa na utaratibu wa kufanya tathmini kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa ghala katika Wilaya mbalimbali ili kubaini mahitaji halisi ya ghala. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, Wizara itafanya tathmini katika Wilaya ya Kwimba ili kubaini mahitaji halisi ya ghala kwa kuzingatia hali ya uzalishaji na mahitaji katika maeneo husika na itafanya maamuzi stahiki juu ya suala hili.