Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 18 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 215 2026-04-28

Name

Zuberi Yahya Mfaume

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza:-

Je, lini wakulima wa ufuta wa Kisaki, Mvuha, Mngazi, Bwakila chini na Selembala waliouza kwa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani watalipwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Yahya Mfaume, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika msimu wa mwaka 2024/2025, wakulima wa ufuta katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro waliuza jumla ya tani 3,984 zenye thamani ya shilingi bilioni 9.841 kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na minada ya kidijiti. Kati ya kiasi hicho, madai ya shilingi bilioni 8.469 yalilipwa kwa wakulima kupitia mfumo huo na shilingi bilioni 1.372 hazikulipwa kwa wakati kutokana na dosari mbalimbali katika mifumo ya malipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufikia mwezi Oktoba, 2025, madai yote ya wakulima waliouza ufuta kupitia mfumo huo yalilipwa kikamilifu katika maeneo ya Mngazi, Selembala, Bwakila Chini, Kisaki na Mvuha. Mfumo huo umeendelea kuongeza uwazi, kuondoa ucheleweshaji wa malipo na kuhakikisha wakulima wanapata stahiki zao kwa wakati. Aidha, Serikali inatoa wito endapo kuna Mkulima ana changamoto katika malipo yake, awasilishe madai yake ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.