Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza:- Je, lini wakulima wa ufuta wa Kisaki, Mvuha, Mngazi, Bwakila chini na Selembala waliouza kwa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani watalipwa?
Supplementary Question 1
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini ninakushukuru kwa kukiri kwamba kulikuwa na malipo ambayo yalichelewa. Kwa kweli tuna changamoto kubwa kwa vyama vya ushirika vya msingi katika kushughulikia uuzaji wa nafaka hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itarasimisha mfumo mbadala na mfumo shindanishi ambao utaleta tija kwa wakulima? La pili, Morogoro Kusini tumekuwa wazalishaji wa ufuta ambao una daraja la juu. Kuna changamoto kubwa ya vifaa vya kilimo pamoja na pembejeo. Ni lini sasa Wizara itapeleka vituo vya ukodishaji matrekta pamoja na kusambaza pembejeo ili kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa wingi zaidi? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza tena Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mheshimiwa Mfaume kwa kufuatilia sana wananchi wake mara kwa mara. Nimwondoe shaka tu kwamba, moja, Serikali ipo karibu sana na kuwasikiliza wananchi kero zao zinapokuwa zinatatuliwa, ndiyo maana katika wiki mbili zilizopita, nilijibu swali la namna hii hapa Bungeni, watu wakiomba tupitie mfumo ili kurekebisha ule upungufu. Kwa hiyo, Serikali tuko tayari kupitia, sisi pamoja na wadau na kuainisha yale maeneo yenye upungufu ili tuweze kuongeza ufanisi katika mifumo hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sisi kama Serikali tuko tayari muda wowote kufanya kazi pamoja ili tuweze kutengeneza mfumo mbadala na shindanishi ambao unaweza kuwasaidia wananchi hao. Kuhusu ni lini tutapeleka matrekta huko na pembejeo, mpango wa Serikali ni kuanzisha vituo vya zana za kilimo katika halmashauri zote nchini. Lengo la Serikali ni kuanzisha vituo 1000, na mpaka sasa hivi tumeshafungua vituo 79 katika halmashauri kama 25 hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mpango huu ni endelevu, na katika mipango inayokuja, Jimbo la Morogoro Kusini lipo katika mpango huo, ahsante sana.
Name
Eric James Shigongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buchosa
Primary Question
MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza:- Je, lini wakulima wa ufuta wa Kisaki, Mvuha, Mngazi, Bwakila chini na Selembala waliouza kwa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani watalipwa?
Supplementary Question 2
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona. Katika historia ya nchi yetu, awamu pekee iliyojenga skimu nyingi za umwagiliaji, ni Awamu ya Sita. Kule kwetu Buchosa zimejengwa skimu za Mwigulukenda, Sukuma. Je, Serikali ina mpango gani kujenga skimu nyingine za umwagiliaji katika mabonde ya Bupandwa, Buchiri na Iseni?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mheshimiwa Shigongo kwamba, maelekezo ya Serikali ambayo Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu alishayatoa, ni kwamba Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ifanye upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwenye mabonde yote nchini. Kazi hiyo inaendelea, ikiwemo maeneo haya ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyaainisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali ni kupata gharama halisi, na baada ya hapo tuweze kutangaza na kupata wakandarasi ambao watatekeleza kazi hiyo. Kwa hiyo, kwa sasa tuko katika hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, na baada ya hapo sasa tutakwenda katika hatua inayofuatia, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved