Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 18 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 217 | 2026-04-28 |
Name
Fadhili Sandali Chilombe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Miradi ya Maji katika Jimbo la Tunduru Kusini?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mhandisi Fadhili Sandali Chilombe, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa jumla ya miradi ya maji sita yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 7.8 katika Wilaya ya Tunduru ikiwemo Jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma. Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Tuwemacho, Masuguru - Mchoteka Awamu I, Misechela - Liwanga, Msinjili na Azimio.
Zijin ya China Miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa vyanzo vya maji, ujenzi wa matanki manne yenye ujazo wa lita 750,000, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 74.1 sanjari na ujenzi wa vituo 25 vya kuchotea maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshalipa jumla ya shilingi bilioni 2.9 kwa miradi hiyo ambapo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na inatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2026/2027 kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved