Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Azza Hilal Hamad

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Miradi ya Maji katika Jimbo la Tunduru Kusini?

Supplementary Question 1

MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakwenda kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Masengwa katika vijiji vya Ibingo, Isela, Bubale, Ng’wang’halanga na Ishinabulandi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana dada yangu, Mheshimiwa Azza, kwa kuendelea kuwasemea vyema kabisa wananchi na kwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ndani ya jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali tumejipanga na tutakwenda kuhakikisha miradi yote inakamilishwa, lakini jambo la kukubaliana ni kwamba tunayo miradi mingi, ni lazima tuwalipe wakandarasi awamu kwa awamu na utekelezaji wa miradi uende awamu kwa awamu kulingana na vipaumbele. Ninamhakikishia Mheshimiwa Azza, mradi wake awamu ya pili tunakwenda kuupatia kipaumbele kwa ajili ya kuutekeleza mara moja. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Josephine Tabitha Chagulla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Miradi ya Maji katika Jimbo la Tunduru Kusini?

Supplementary Question 2


MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona ili niulize swali langu la nyongeza. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Nyang’hwale? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Josephine, ninaomba uulize tena swali lako.
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona ili niulize swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Nyang’hwale? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kutoka Mkoa wa Geita. Ninapenda kumpongeza kwa kazi nzuri sana ambayo anaendelea kuifanya na kuwasemea wananchi wa mkoa mzima wakiwemo wananchi wa Wilaya ya Nyang’hwale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo miradi mingi inayoendelea ndani ya Jimbo la Nyang’hwale na ipo katika hatua nzuri. Pia, mpaka sasa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama ni wa kuridhisha sana ndani ya jimbo hilo. Bahati nzuri mimi nimeshafanya ziara pale nikajionea na tukasimamia utekelezaji wa miradi iliyokuwa inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna miradi ambayo tayari imeshakamilika na kuna miradi ambayo inahitaji kumaliziwa kwa kupelekewa fedha tu. Ikishakamilika, basi upatikanaji wa huduma ya maji utakuwa zaidi ya 85%. Ninakushukuru sana.

Name

Amina Mussa Mkumba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Miradi ya Maji katika Jimbo la Tunduru Kusini?

Supplementary Question 3

MHE. AMINA M. MKUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itatenga bajeti ili kuanzisha miradi katika Jimbo la Kibiti katika maeneo ya Visiwani ambapo kuna kata nne: Kata ya Kiongoroni, Mbuchi, Maparoni na Msala? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijue ni jimbo au wilaya gani, kwani ni kata tu amezitaja.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Amina, ninaomba uulize swali lako tena, lakini tunaomba Waheshimiwa Wabunge tupunguze sauti ili tuweze kusikilizana.

MHE. AMINA M. MKUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Swali langu linauliza, ni lini Serikali itaanzisha miradi katika Jimbo la Kibiti, maeneo ya Visiwani ambapo kuna Kata nne za Msala, Maparoni, Kiongoroni na Mbuchi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kutekeleza miradi yote na kuikamilisha ili iweze kutoa matokeo kwa wananchi. Pia, ni dhamira ya Serikali ya CCM ambapo falsafa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kumtua mama ndoo kichwani. Hapo ni Sera yetu ya Maji ya Mwaka 2002 ambapo toleo la mwaka 2025 linatutaka kuhakikisha kwamba maji yawe siyo zaidi ya meta 400.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, dhamira hiyo hiyo inatusukuma kuhakikisha kwamba tunaweka msukumo kwenye kupeleka fedha ili miradi mbalimbali iendelee kutekelezwa ikiwemo na miradi ambayo Mheshimiwa Mbunge ameiongelea, Tutakwenda kuipatia msukumo mkubwa ili iweze kutekelezwa na kukamilika na kutoa matokeo na wananchi ambao wamemtuma kuwasemea ili sauti yako iweze kutambulika kwa matokeo zaidi ambayo yatakuwa yametokea katika jimbo lake. Ahsante sana.