Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 496 2026-06-03

Name

Thomas Maganga Kampala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: -
Je, lini miundombinu ya Shule ya Mkondo wa Amali Mulele itajengwa ikiwemo nyumba ya walimu na karakana za ufundi wa magari na umeme?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Thomas Kampala Maganga, Mbunge wa Jimbo la Katavi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka 2023/2024 Serikali ilipeleka shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya amali katika Halmashauri ya Mlele ambapo shule hiyo imejengwa katika Kata ya Utende. Miundombinu iliyojengwa ni pamoja na madarasa nane, jengo la utawala moja, maktaba moja, maabara mbili, chumba cha TEHAMA kimoja, bwalo moja, mabweni manne, karakana moja, nyumba ya mwalimu moja, matundu ya vyoo nane, kichomea taka kimoja na tanki la ardhini kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa shule hii umekamilika na shule imesajiliwa kwa jina la Shule ya Sekondari Mgombe Amali ya Kihandisi. Shule hii ina wanafunzi 63; wavulana 38 na wasichana 25 wanasoma amali za ufundi bomba, ufundi magari, ufundi umeme na magari na mfumo wa umeme wa jua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kujenga shule za amali ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya amali. Ahsante.