Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini miundombinu ya Shule ya Mkondo wa Amali Mulele itajengwa ikiwemo nyumba ya walimu na karakana za ufundi wa magari na umeme?
Supplementary Question 1
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninashukuru pia kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo shule ya amali ambayo inajengwa katika Jimbo la Mlalo pale Tarafa ya Mlalo katika Kata ya Mwangoi. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule ile?
Mheshimiwa Mwenyekiti, upo mpango wa kupeleka shule za amali katika majimbo ambayo hayakufanikiwa kupelekewa Vyuo vya VETA. Je, uko mpango wa kupeleka shule mahsusi ya ufundi kwa maana ya amali katika Jimbo la Bumbuli? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali kupitia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 imeweka mkakati madhubuti kuhakikisha kwamba tunaboresha elimu ya sekondari kwa maana ya mafunzo ya amali na kihandisi na ndio maana Serikali imeanzisha shule 103 na kati ya shule hizo, shule 29 ni za amali za kihandisi, lakini shule 74 ni za mafunzo ya amali kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameongelea shule ya amali katika Jimbo la Mlalo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ilipeleka fedha awamu ya kwanza takribani shilingi milioni 583 kwa ajili ya ujenzi wa majengo awamu ya kwanza na majengo hayo kote nchini yamekamilika na yako machache yako hatua za mwisho za ukamilishaji, na hatua inayofuata ni ujenzi wa awamu ya pili. Serikali inaanda taratibu za kibajeti kwa ajili ya kupeleka fedha ili tuweze kukamilisha majengo hayo.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Sekiboko kwamba tutahakikisha pia jengo au shule ya amali katika Jimbo la Mlalo linapelekewa fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, kuhusiana na ujenzi wa shule za amali kwenye majimbo ambayo hayana VETA ikiwemo Jimbo la Bumbuli, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea. Kwanza kufanya tathmini, lakini pili kuendelea kuainisha maeneo ambayo ni muhimu kujengewa shule za amali na tutahakikisha pia tunatoa kipaumbele katika Jimbo la Bumbuli.
Name
Alan Thomas Mvano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kakonko
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini miundombinu ya Shule ya Mkondo wa Amali Mulele itajengwa ikiwemo nyumba ya walimu na karakana za ufundi wa magari na umeme?
Supplementary Question 2
MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, na mimi nipongeze jitihada hizi nzuri za Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Wilaya ya Kakonko 60% ilionesha kuwa na watoto, 30% vijana na 10% wazee. Sasa kwa muktadha huo katika Wilaya ya Kakonko hatuna shule ya amali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni upi sasa mpango wa Serikali kwa kuzingatia kundi hili kubwa la 60% ya wananchi wa Kakonko ambao bado ni watoto wa kujenga shule ya amali katika Wilaya ya Kakonko ili kuweza kuwajengea uwezo na kuhakikisha wanakuwa wakiwa na elimu bora katika mazingira yetu? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, katika utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa shule za sekondari za amali kwanza Serikali ilitoa kipaumbele kwa halmashauri au wilaya ambazo hazina Vyuo vya VETA, lakini kwa sababu ya dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, sasa wilaya zote zinaendelea na ujenzi wa VETA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa muktadha huo tuna uhakika kwamba Wilaya ya Kakonko pia itapata Chuo cha VETA lakini wakati huo huo tutaangalia uwezekano wa kutenga fedha kwa ajili ya kujenga shule za amali katika Jimbo la Kakonko. (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini miundombinu ya Shule ya Mkondo wa Amali Mulele itajengwa ikiwemo nyumba ya walimu na karakana za ufundi wa magari na umeme?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Shule ya Sekondari ya Ihanda ilichaguliwa kuwa ni mojawapo ya shule ambayo ingeweza kujengewa miundombinu ya mafunzo ya amali. Ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kuanza kujenga miundombinu hiyo? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ziko shule ambazo zimekwishaainishwa kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Vwawa kwamba tuna mpango wa kuendelea kuandaa bajeti kwa awamu ili kuendelea kujenga majengo yatakayoziwezesha baadhi ya shule kupata hadhi ya kuwa pia na mafunzo ya amali.
Kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kuipa kipaumbele shule hiyo kwa kadri ya bajeti zetu na kwa kadri ya tathmini ya vigezo ili tuweze kuona uwezekano wa kuongeza majengo ya mafunzo ya amali katika shule hiyo ya sekondari. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved